Breaking News

Coutinho kuwa nje ya uwanja kwa wiki 6






Habari mpya.Mchezaji tegemeo wa klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho anategemea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma 6 baada ya kupata majeraha.
Mchezaji huyo amepata jeraha kwenye kifundo cha mguu wakati akiitumikia klabu yake ya Liverpool kwenye mchezo dhidi ya Sunderland kwenye ligi kuu ya Uingereza katika mchezo ambao Liverpool walipata ushindi wa magoli 2-0.Mchezaji huyo alipata majeraha hayo kipindi cha kwanza na kumfanya kushindwa kuendelea na mchezo huo.

 

 Hata hivyo Liverpool wana matumaini kuwa mchezaji wao huyo atarejea uwanjani mapema zaidi kuliko muda huo uliokadiriwa kupona majeraha yake.

    KILALA KHERI KWA COUTINHO.

No comments