Breaking News

Riyad Mahrez ashinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika




Riyad Mahrez ametawazwa kuwa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC wa Mwaka 2016.
Mashabiki kutoka kila pembe ya dunia walimpigia kura nyingi kiungo huyu wa kati wa Algeria na Leicester kuliko Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.
Mahrez ameambia BBC Sport: "Naam, [tuzo hii] ina maana kubwa sana kwa sababu bila shaka mimi ni Mwafrika na ni jambo kuu sana kwa mchezaji wa Afrika nafikiri, kwa hivyo nina furaha isiyo na kifani, najivunia kuipokea.."

Tuzo hii ni kilele kwenye mwaka mzuri kwa mchezaji huyu wa miaka 25, ambaye tayari amejishindia taji la Ligi ya Premia na alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la Wachezaji Uingereza.
Mahrez ametambuliwa kwa uchezaji wake mzuri kama mchawi katika wingi, ambaye familia yake inatoka kijiji kidogo kwa jina El Khemis nchini Algeria, ambaye alitikisa Ligi ya Premia.
Alisaidia sana Leicester City kushinda ligi bila kutarajiwa, ambapo alifunga mabao 17 na kusaidia ufungaji wa mabao 11 kuwawezesha kushinda, licha ya uwezekano wao kushinda mwanzoni mwa msimu kuwa 5000-1 pekee.


No comments