Breaking News

Diwani ajivua madaraka kupinga ubadhirifu




Mmoja wa madiwani wa Manispaa ya Shinyanga amebwaga manyanga kwenye kamati akiwatuhumu wenzake kwa ubadhirifu.



Diwani huyo wa Ndembezi, David Nkulila (CCM) amejiuzulu ujumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala huku akiituhumu kwa ubadhirifu wa fedha za umma.



Nkulila amesema amefikia uamuzi huo kutokana na kuwapo ubadhirifu wa fedha hizo na udanganyifu unaofanywa katika

ujenzi wa barabara kwa kuongeza kilomita tofauti na uhalisia.



Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, Lewis Kalinjuna akizungumza kwa simu, amesema kwa sasa hana muda wa kujishughulisha na mambo hayo zaidi ya maendeleo.



 Amesema anayetakiwa kutoa majibu ni diwani mwenyewe kwa sababu ni mjumbe wa kamati hiyo.



Hata hivyo, Nkulila amesema hayupo tayari kuunga mkono uozo unaoendelea na kuzitaka mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mchakato wa ununuzi ya greda lililogharimu Sh520 milioni.



Meya wa manispaa hiyo, Gulamhafeez Mukadam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala amesema hajapokea barua ya kujiuzulu kwa mjumbe huyo.

No comments