Breaking News

Dan Alves atabadili namba ya jezi yake mechi dhidi ya Argentina,hii ndiyo sababu.


Beki wa kulia wa timu ya taifa ya Brazil Dan Alves atabadili namba ya jezi yake iliyozoeleka kwenye mechi dhidi ya Brazil na Argentina.Mechi hiyo inategemewa kupigwa katika hatua za kutafuta kufuzu kombe la dunia mwaka 2018.
  Beki huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na sasa akiitumikia Juventus ya Italia atabafili namba ya jezi yake kwenye mechi hiyo na kuvaa jezi namba 4 ili kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa taifa wa Brazil Carlos Arberto ambaye anatajwa kuwa nini miongoni wa wachezaji bora waliwahi kutokea Brazil.Mchezaji huyo amefariki mwezi uliopita akiwa na miaka 72.

Moja ya tukio kubwa analokumbukwa mchezaji huyo ni kufunga goli mhimu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1972

No comments