Breaking News

TB Joshua aondoa utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook



Utabiri uliofanywa na muhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua kwmba Hillary Clinton atashinda uchaguuzi wa urais nchini Marekani umeondolewa katika akaunti yake ya facebook.
Bwana Joshua aliwaambia wafuasi wake siku ya Ijumaa kwamba ameona mwanamke akishinda.
Baada ya Donald Trump kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa Jumanne ,wageni katika ukurasa wa facebook wa Muhubiri huyo walishangaa walipoona utabiri huo umeondolewa.

No comments