Breaking News

Hivi ndiyo vipaumbele vya Trump,pia afuta kuwazuia waislamu




Baada ya mkutano na msemaji wa Republican Paulo Ryan, rais mteule wa Marekani Bwana Donald Trump ameeleza vipaumbele vya sera zake.
Mteule huyo amesema atapunguza kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na mfumo uliowekwa na Barack Obama.
Pia amesema atabadili haraka sheria juu ya uhamiaji , Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.
  Alisema yeye atafanya mambo ya kuvutia kwa ajili ya watu wa Marekani. Lakini baadhi ya ahadi alizotoa kwenye kampeni zimeondolewa kwenye tovuti yake ikiwemo tishio la kupiga marufuku Waislamu kuingia Marekani, kuachana na makubaliano ya Paris katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

No comments