Breaking News

Iwobi ana matumaini kuwa Arsenal itaifunga PSG na kuongoza kundi

Image result for iwobi 300 pxl

Winga wa klabu ya Arsenal ya uingereza Alex Iwobi ametamba kuwa kwasasa klabu hiyo ina uwezo wa kuifunga klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na kuongoza kundi A ambalo timu hizo mbili zinaonekana kuwa ndiyo zenye nguvu na ushindani mkubwa.
  Hayo yanafuatia kiwango kizuri ambacho kimeonyeshwa na klabu hiyo kwenye mechi za hivi karibuni huku jana ikipata ushindi mkubwa kwa kuifunga klabu ya Ludogorets mabao 6-0 ikiwa ni mechi ya klabu bingwa barani ulaya.
  Ikumbukwe klabu hizo mbili zilikutana kwenye mzunguko wa kwanza mechi ambayo ilichezwa nchini Ufaransa na matokeo yakawa 1-1 na hivyo kuifanya mechi ya marudiano ambayo itafanyika nchini Uingereza kuwa ngumu zaidi.
    Pia mchezaji huyo hakuacha kuwazungumzia wachezaji wenzie huku akisisitiza kuwa klabu hiyo imejaa vipaji vyenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira na huku akimsifu mchezaji Alex Chamberlain ambaye katika mechi ya jana alikuwa kwenye kiwango bora huku akifanikiwa pia kufunga goli.

No comments