Uganda yawakamata wafuasi wa Donald Trump
Taarifa zinasema kuwa, raia wawili wa Uganda wamekamatwa Jumanne walipokuwa wakiandamana nje ya ubalozi wa Marekani mjini Kampala wakimuunga mkono Donald Trump.
Taarifa zinasema wawili hao walikuwa na mabango yaliyokwa yameandikwa kuwa: "kumpigia kura Trump ni kura dhidi ya udikteta Afrika."
Watu hao wawili waliokamatwa wametambuliwa kuwa ni Bigirwa Moses na Allan Kitonsa ambao ni wanachama wa tawi la vijana la Chama cha Kidemokrasia cha Uganda, UDP.
Msemaji wa polisi Uganda Bi. Emilian Kayima amesema yamkini wawili hao wakafunguliwa shtaka la mjumuiko ulio kinyume cha sheria. Ubalozi wa Marekani mjini Kampala umethibitisha kutokea tukio hilo pasina kutoa maelezo zaidi.
Uchaguzi wa Rais wa Marekani utafanyika November 8, mwaka huu wa 2016.

No comments