Breaking News

Watu 12 wameuawa kwa shambulio la kigaidi Mandera,Kenya




Watu kadha wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la malazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Maafisa wa polisi wamesema watu 12 wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa.
Polisi na wanajeshi kwa sasa wanafanya msako na kushika doria mjini.
Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.
Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali.

No comments