Edin Dzeko atolewa kwa kadi nyekundu kwa kumvua bukta mchezaji mwenzie
Mvhezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Manchester city na timu ya taifa ya Bosnia Edin Dzeko amefanya tukio la kijinga na lisilo la kiungwana baada ya kumvua kaptura mchezaji mwenzake kwenye mechi kati ya Bosnia na Ugiriki.
Tazama video hapa chini ya tukio hilo.
Dzeko alilifanya tukio hilo kwa mchezaji Kyriakos Papadopoulos aliyekuwa akijaribu kuchukua mpira kutoka kwa mchezaji huyo ambaye wakati huo alikua chini.Dzeko alikua katika harakati za kumzuia mchezaji huyo kwa kuhisi hakutendewa haki baada ya kuanguka na zoezi lake la kumzuia liliposhindikana akaamua kumvua bukta mvhezaji huyo na kumwacha nguo ya ndani ikionekana.Kwa kitendo hicho mwamuzi wa mchezo huo hakua na maamuzi mengine zaidipya kumpa kadi nyekundu mchezaji huyo.

No comments