Madiwani wacharuka kutetea leseni za waganga wa jadi
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wamembana Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Beatus Chikoti wakidai maelezo kwa nini waganga wa jadi 630 hawajapewa leseni licha ya kuzilipia miaka mitatu iliyopita.
Hoja hiyo iliibuliwa juzi na Diwani wa Chinamili, Nindwa Sitta aliyehoji zilipo zaidi ya Sh12.8 milioni zilizolipwa na waganga hao na wasaidizi wao kwa ajili ya leseni za kazi.
“Madiwani tulikuwa mstari wa mbele kuwahimiza waganga katika kata zetu kujisajili kutekeleza agizo la Serikali, hivi sasa wanatuhoji vilipo vibali vyao na hatuna majibu. Leo tunakata mganga mkuu atueleze zilipo leseni za waganga hawa,” alihoji diwani huyo.

No comments