Mahakama yataka Neymar kufungwa miaka 2 jela
Waendesha mashtaka nchini Uhispania
wamemtaka mshambuliaji wa Barcelona Neymar kuhudumia kifungo cha miaka
miwili jela kufuatia kuhusika kwake katika kesi ya ufisadi kuhusu
uhamisho wake kutoka klabu ya Santos nchini Brazil mwaka 2013.
Jaji
Jose Perals pia ametaka aliyekuwa rais wa Barcelona sandro Rosell
kuhudumia kifungo cha miaka mitano jela mbali na kupigwa faini ya Yuro
milioni 7.2 kwa klabu hiyo.Imetaka kutupiliwa mbali kwa mashtaka dhidi ya rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria bartomeu.
Rosell,Neymar na babake wanatarajwa kushtakiwa.
Kesi hiyo inatokana na malalamishi ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS ,ambalo linamiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar na linadai lilipata fedha chache ikilinganishwa na zile lililotarajia.
Rosell alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mwaka 2014 kwa jukumu lake katika uhamisho huo na kutoa ushahidi mahakamani mnamo mwezi Februari pamoja na Bartomeu,Neymar na babake Neymar
No comments