Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo (Ijumaa), baada ya afya yake kuimarika. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa imesema kuwa kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema. "Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru madaktari na wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara. "Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth. Mama Janeth alilazwa MNH tangu juzi baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.
Mwanamke mfuasi wa chama cha Democratic ambaye alivunjwa moyo na kushindwa na Bi Hillary Clinton amekutana na mtu asiyemtarajia porini, mgombea huyo mwenyewe.
Margot Gerster alienda matembezi akiwa na binti yake na mbwa katika msitu wa Chappaqua, New York.
Hakutarajia kukutana na Bi Clinton ambaye alishindwa na Donald Trump wa Reublican siku mbili awali, lakini hilo ndilo lililotokea.
Picha yake pamoja na Hillary Clinton ndiyo mara ya kwanza Bi Clinton kuonekana hadharani tangu atoe hotuba ya kukubali kushindwa Jumatano.
Bi Gerster anasema picha hiyo ilipigwa na mumewe Hillary Clinton, Bill.
Bi Gerster, ambaye huishi White Plains, amesimulia kuhusu kisa hicho kwenye Facebook.
Ujumbe wake ulipendwa mara zaidi ya 110,000 na kusambazwa na watu 9,000 kabla yake kuufanya wa faraghani.
"Nilimkumbatia na kuzungumza naye na kumwambia kwamba moja ya nyakati ninazojivunia zaidi kama mama ni wakati ambao nilimbeba Phoebe nikaenda naye na tukampigia kura," amesema.
"Alinikumbatia na kunishukuru na tukasemezana na kisha nikamwacha aendelee na matembezi."


No comments