Breaking News

Mtandao mpya wa kijamii waanzishwa Nigeria,kupambana na facebook.


Linda Ikeji mwanamitindo wa zamani wa nchini Nigeria kutoka jiji la Lagosi amefungua ukurasa mpya katika huduma za internet kwa kuanzisha mtandao wa kijamii uitwao Linda Ikeji Social ambao amedhamiria kushindana na mtandao wenye nguvu duniani wa facebook.
Mtandao huo ambao ndani ya masaa 24 tangu kuanzishwa kwake tayari ulikuwa na watu 50,000 waliojiunga nao.Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa mtandao huo mwadada huyo alisema watu wengi kwasasa wanahangaika kupitia mitandao mbali mbali kwaajili ya kusoma habari,kununua vitu na pia kubadilishana maoni.
 Mwanadada huyu ambaye pia ni mwanablog mashuhuri wa habari nchini Nigeria kwenye mtandao wake huo wamekusudia kuwalipa fedha watumiaji zaidi wa mtandao huo..

         Tunamtakia kila la kheri!!


No comments