RC Kagera aanza kutoa misaada ya tetemeko
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu amezindua mpango wa kutoa vifaa vya ujenzi kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililitokea miezi miwili iliyopita.
Akizindua zoezi hilo katika ofisi za Kata ya Kashai, Meja Jenerali Kijuu amesema kuwa mpango huo katika awamu ya kwanza ya kutoa mabati 20 na mifuko mitano ya saruji utanufaisha kaya 200 kati ya 370 zilizolengwa.
Mpango huo utanufaisha kwanza makundi maalumu ya wazee, walemavu, yatima na wajane.
Kwa kuanzia mkuu wa mkoa amekabidhi msaada huo kwa Imelda Kiiza (95) katika mtaa wa Lwome, huku akisisitiza wananchi wenye uwezo waanze kujenga nyumba zao wenyewe na Serikali itawakuta njiani.RC Kagera aanza kutoa misaada ya tetemeko

No comments