Real Madrid yaitwanga Atletico Madrid 3-0.
Atletico Madrid wamedhihirisha kuwa wao sio tishio tena mbele ya Real Mad7id baada ya jana kuruhusu kuendelea kufungwa na miamba hao wa Hispania mabao 3-0.
Katika mchezo huo Real madrid walionekana kuutawala zaidi na dakika ya 23 walifanikiwa kupata mpira wa adhabu ambao ulipigwa na mwanandinga ambaye ana nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Christian Ronaldo ma kuiandikia madrid goli la kuongoza.
Magoli mengine yalifungwa dakika ya 71 kwa njia ya penati iliyofungwa na mreno huyo pia goli la tatu dakika ya 77 liliwekwa nyavuni kupitia mguuni kwake na hivyo kuwa amefunga hatrick mara mbili kwenye uwanja huo wa vicente calderon.Hiyo ilikuwa hatrick ya 39 kwa Ronaldo akiwa Hispania na ya 44 katika maisha yake ya soka.Kwa matokeo hayo madrid wameendelea kukaa kileleni na wakiwaacha Barcelona kwa poini 5 ambao jana walitoka 0-0 dhidi ya Malaga.
No comments