Samia asafiri na ATCL kwenda Mwanza
Serikali ya awamu ya tano imeendelea na hatua yake ya kupunguza matumizi baada ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kusafiri na msafara wake kwa ndege ya ATCL.
Safari hiyo ambayo ilihusisha maofisa 16 wa Serikali imegharimu Sh7.6 milioni badala ya Sh40 milioni ambazo zingetumika kukodi ndege.
Akizungumza kabla ya kupanda ndege hiyo, Samia alisema ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha huduma za ATCL.
"Nimeamua kusafiri na ndege hii pamoja na msafara wangu huu ili kuunga mkono juhudi za Serikali yetu kwa ATCL, pia uzalendo na kupunguza gharama za matumizi hapa tungesafiri kwa ndege ya kukodi tungetumia takribani Sh40 milioni," alisema.
Samia alipanda ndege hiyo saa 9 jioni alitarajiwa kuwasili Mwanza saa 10.20 jioni.

No comments