Breaking News

Wazimbabwe waifinyanga taifa stars 3-0


TAIFA STARS Leo huko Uwanja wa Taifa Jijini Harare wametandikwa 3-0 na Wenyeji wao Zimbabwe katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki ambayo iko kwenye Kalenda rasmi ya FIFA na bila shaka itazidi kuiporomosha kutoka Listi ya FIFA ya Ubora Duniani.

Hadi Mapumziko, Stars, Chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa, walikuwa nyuma kwa Bao 1-0 lilifungwa na Knowledge Musona anaecheza Soka huko Belgium.

Dakika za 53 na 56 Zimbabwe walipiga Bao 2 zaidi kupitia Rusike na Mushekwi.

Stars walikuwa nae Nahodha Mbwana Samatta na pia Thomas Ulimwengu kuingizwa baadae lakini Mapro hao hawakufurukuta.

VIKOSI:

ZIMBABWE: Mukuruva Tatenda, Zvirekwi Hardlife [Oscar Machapa, 73’], Bhasera Onismo [Kangwa, 73’], Phiri Danny, Hadebe Teenage, Katsande Willard, Nakamba Marvelous, Rusike Matthew, Mahachi Kudakwashe [Malajila, 73’], Musona Knowledge [Tinotenda Kadewere, 71’], Mushekwi Nyasha

TAIFA STARS: Aishi Manula, Michael Aidan, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Andrew Vincent, Himid Mao, Simon Msuva [Thomas Ulimwengu, 69’], Mzamiru Yassin [Mohammed Ibrahim, 69’], Mbwana Samatta, Elius Maguri [John Bocco, 72’], Shiza Kichuya

No comments