Breaking News

Dkt. Mwakyembe asema ubadhilifu,wizi,rushwa na ufisadi wachangia Kudidimiza uchumi .



Waziri wa katiba na sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema ubadhilifu,wizi,rushwa na ufisadi umechangia kwa kiasi kikubwa Kudidimiza ukuaji wa uchumi  wa nchi  na  hivyo kusababisha hali ya  umasikini  kwa wanachi  walio wengi  huku wachache Wakineemeka na ndio maana serikali ya  awamu ya tano haipo tayari kuona rushwa inapata nafasi kwa njia yoyote ile.
Mh.Mwakyembe  ameyasema  hayo  katika   uzinduzi wa wiki ya kutoa  huduma  kwa wananchi katika kuadhimisha  siku ya  maadili Kitaifa na haki za binadamu ambapo amesema rushwa kwa sasa haina nafasi tena. Naye waziri wa  nchi ofisi ya  rais na utawala bora Mh. Angelah Kairuki amesema  sheria na kupambana na rushwa inatoa adhabu Ndogo kwa wale wanaobainika na hivyo kulisasabishi hasara taifa  na hivyo wanataka sheria hiyo imbane mhusika kulipa hata hasara zilizotokana na kosa lake.

Valentino Mlowola ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU amesema  wamekuwa wakipokea taarifa nyingi za watu wakilalamikia utendaji wa ofisi za serikali  na  utekelezaji wa viwango vya chini wa  miradi ya umma huku  mwenyekiti wa  tume ya haki za binadamu  na utawala bora Mh. Tom Bahame Nyanduga  akisisitiza  watendaji kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi wao

No comments