Breaking News

Ibrahamovich na Pogba wameipa ushindi Manchester united.


klabu ya aoka ya Manchestee united ya nchini Uingeeeza imepata ushindi wake wa pili mfululizo baada ya kuifunga Crystal Palace magoli 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza uliofanyika usiku wa kuamkia leo.
Goli la kwanza la Man utd lilifungwa na kiungo wa klabu hiyo aliyesajiliwa kwa rekodi ya Dunia Paul Pogba zikiwa zimesalia dakika 2 kuelekea mapumziko.
Dakika ya 66 Palace walisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji JMcArthur kabla ya mkongwe Zlatan Ibrahamovich kuongeza goli la pili katika dakika ya 88 na kuihakikishia Man utd kupata alama 3 muhimu katika mtifuano wa ligi kuu Uingereza.

Vikosi vilivyoshiriki mechi hiyo na alama alizozipata kila mchezaji kwenye mechi hiyo kufuatia uwezo aliouonyesha


Crystal Palace: Hennessey (6), Ward (6), Dann (6), Delaney (7), Kelly (6), McArthur (7), Flamini (5), Lee (5), Cabaye (5), Zaha (6), Benteke (5).

Used subs: Campbell (n/a), Ledley (5), Fryers (5).

Man Utd: De Gea (8), Bailly (6), Jones (7), Rojo (5), Blind (7), Herrera (7), Carrick (7), Pogba (9), Mata (6), Ibrahimovic (8), Rooney (6).

Used subs: Lingard (5), Rashford (5), Darmian (6).

Man of the Match: Paul Pogba.

No comments