Breaking News

Mahakama yamwachia Ole Sabaya, akamatwa tena




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imemwachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha (UVCCM), Lengai ole Sabaya baada ya mawakili wa Serikali kuitaka mahakama hiyo ifute shauri hilo, kwa kuwa hawana lengo la kuendelea na kesi hiyo.

Sabaya alikuwa akituhumiwa kujifanya mtumishi wa umma, Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na ilidaiwa alikamatwa na nyaraka za kughushi za TISS. Hata hivyo, Sabaya baada ya kauchiwa huru, alikamatwa tena na Polisi nje ya viwanja vya mahakama hiyo.

Wakili wa serikali katika kesi iliyokuwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga, Grace Madikenga alidai mahakamani hapo kuwa upande wa serikali hauna lengo la kuendelea na kesi hiyo hivyo wanaiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.

Kesi hiyo jana ilitarajiwa kusikilizwa ambapo shahidi wa kwanza wa upande wa serikali, Inspekta Rogathe alitarajiwa kutoa ushahidi wake.

“Leo kesi ilikuwa ianze kusikilizwa ila upande wa serikali hatuna nia ya kuendelea na kesi hii hivyo tunaiomba mahakama iifute,” alidai Madikenga.

Kufuatia maombi hayo ya upande wa serikali, Hakimu Gwantwa alikubaliana na maombi hayo na kuifuta kesi kisha mahakama hiyo ilimwachia huru mtuhumiwa huyo.

Ole Sabaya alikuwa akikabiliwa na mashitaka mawili katika kesi hiyo ambapo kosa la kwanza ni kudaiwa kujifanya mtumishi wa umma ambapo Mei 18 mwaka huu hoteli ya Sky way iliyopo makao mapya Jijini Arusha alijifanya kuwa mwajiriwa wa Usalama wa Taifa (TISS).

Kosa la pili katika siku isiyofahamika wala tarehe mwaka huu alighushi nyaraka za kitambulisho cha usalama wa Taifa chenye picha yake na kutumia namba Saturday. Code. Eagle 3 idara ya usalama wa Taifa chenye namba MT. 86117 Sabaya akikamatwa saa 4:53 asubuhi ambapo aliondolewa mahakamani hapo na gari la polisi lililokuwa na namba za usajili T 953 CSZ.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Sabaya amekamatwa kwa kesi hiyo hiyo na kuwa wanafanya taratibu na watakapomaliza atafikishwa tena mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabil

No comments