Matteo Renzi ajiuzulu baada ya kushindwa kura ya maamuzi Italia
Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi
amejiuzulu baada ya kukubali kushindwa katika kura ya maamuzi kuhusu
marekebisho ya katiba nchini humo.
Akihutubia wanahabari usiku,
kiongozi huyo alisema anakubali lawama kutokana na matokeo hayo, na
kwamba kambi ya La, ambayo ilipinga mageuzi hayo, sasa inafaa kutoa
mapendekezo ya mwelekeo kutoka sasa.Baada ya sehemu kubwa ya kura kuhesabiwa, kambi ya La inaongoza kwa 60% dhidi ya 40% za Ndio.
Waliojitokeza kupiga kura walikuwa takriban 70% ya wapiga kura wote waliojiandikisha, jambo linalotazamwa na wengi kama ishara yao kuonesha kutoridhishwa kwao na waziri mkuu huyo.
"Kila la heri kwetu sote," Bw Renzi aliwaambia wanahabari.
Alieleza kuwa ataitisha mkutano wa baraza la mawaziri baadaye adhuhuri Jumatatu.
Baadaye, atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais wa Italia, baada ya kuhudumu kwa miaka miwili unusu.
Bw Renzi alisema mageuzi aliyokuwa amependekeza yangeunguza urasimu mwingi nchini Italia na kuifanya kuwa na ushindani zaidi.
Lakini kura hiyo ya maamuzi ilitazamwa na wengi kama fursa ya kueleza kutofurahishwa kwao na waziri mkuu huyo.
Aidha, kura hiyo ya maamuzi ilitazamwa kama kipima joto cha hisia za kupinga mfumo wa kawaida wa utawala barani Ulaya.
Chama cha Five Star Movement, kilichoongoza kampeni hiyo kimesema kinajiandaa kutawala Italia sasa kufuatia kujiuzulu kwa Bw Renzi. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa mchekeshaji Beppe Grillo.
"Kuanzia kesho, tutaanza kufanyia kazi serikali ya Five Star," mmoja wa viongozi wake, Luigi Di Maio, alisema.
Kiongozi wa upinzani Matteo Salvini, wa chama cha Northern League kinachowapinga wahamiaji, alitaja kura hiyo ya maamuzi kama "ushindi wa raia dhidi ya nguvu zinazodhibiti robo tatu ya dunia."
Vyama vingine vya mrengo wa kulia barani Ulaya vimefurahia matokeo hayo.
Kiongozi wa chama cha Front National nchini Ufaransa, Marine Le Pen, amekipongeza chama cha Northern League kupitia Twitter.
"Wataliano wamejitenga na EU na Renzi. Lazima tutegee sikio kiu hii ya mataifa kutaka kuwa huru," alisema.
Thamani ya sarafu ya euro ilishuka mara moja baada ya matokeo ya mapema kutangazwa.
Kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uthabiti wa Italia kisiasa, taifa ambalo ni la tatu kwa ukubwa kiuchumi katika mataifa yanayotumia sarafu ya euro.

No comments