Breaking News

Mourinho amewalaumu wachezaji wake kutomsikiliza

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester united Jose Mourinho amewatupia lawama wachezaji wake kwa kucheza mchezoi mbovu na kusababisha mipira mingi kupotea na kuwapa nafasi wapinzani kucheza vizuri katika dakika za lala salaama kwenye mchezo wa michuano ya EUROPE ambao uliisha kwa mashetani wekundu hao kushinda magoli 2-0 dhidi ya Zorya.
 Katika mchezo huo magoli ya Manchester united yalifungwa na kiungo aliyeanza kwa mikosi klabuni hapo Henrikh Mkhitaryani na Zlatan Ibrahamovich na kuisaidia klabu hiyo kufuzu kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
  Akizungumza baada ya mechi kocha Mourinho amesema wachezaji wake hawakumsikiliza maelekezo yake kwani katika dakika 15 hizo za mwisho aliwwagiza wachezaji wake hao kukaa na mpira na kuepusha kupoteza mipira ovyo.Aliendelea kusema kuwa walikuwa wakiongoza kwa magoli mawili lakini wakiwa wanacheza mpira mbovu na kupoteza mipira mingi kitu kilichopelekea wachezaji wawili Ander Herrera na Baily kupata kadi za njano na hivyo kuwafanya kuwa hatarini kukosa baadhi ya michezo iwapo watapata tena kadi za njano mechi ijayo.

No comments