habari mpya za kitaifa,kimataifa,burudani,michezo,teknolojia kupitia blog hii mpya kabisa.bongofleva mpya,bunge,Magufuli,waziri,mkuu,blog,muziki,habari afrika,dunia
awala za kijamaa zilianguka kote
duniani , lakini Castro aliendelea kupeperusha bendera nyekundu karibu
na maadui wake wakubwa, Marekani.
Kiongozi huyo mwenye utata
alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa
ambaye aliirejesha Cuba mikononi mwa watu.
Lakini alikabiliwa na
shutuma kwa kuwazima wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na
sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba.
Fidel Alejandro Castro
Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya
mkulima bwanyenye , Angel MarÃa Bautista Castro y Argiz, ammbaye
alihamia Cuba kutoka Uhispania.
Mama yake , Lina Ruz González
alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa
mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa
mkewe. Batista (Kushoto) aliungwa mkono na Marekani
Castro alisoma katika shule ya kikatoliki mjini
Santiago kabla ya kujiunga na chuo kinachoendeshwa na makasisi wa
Jesuit- kilicho El Colegio de Belen jijini Havana.
Hata hivyo, alishindwa kimasomo , na badala yake alipendelea kutumia muda wake mwingi katika shughuli za michezo.
Ilikuwa
wakati anasomea sheria katika Chuo Kikuu cha Havana kati kati ya
miaka ya -1940s ndipo alipokuwa mwanaharakati wa siasa, na kuimarisha
ujuzi wake wa kuzungumza hadharani.
Malengo yake yalikuwa
ni pamoja serikali ya Cuba, iliyoongozwa na Ramon Grau, ambayo
ilikumbwa na shutuma za ufisadi wakati huo.
Ghasia za maandamano ya upinzani ziligeuka kuwa maisha ya kila siku na Castro akajipata akilengwa na polisi.
Pia
alikuwa miongoni mwa watu waliopanga njama za mapinduzi ya kumg'oa
mamlakani Rafael Trujillo, kiongozi wa mrengo wa kulia wa Dominican
Republic , lakini jaribio hilo lilishindwa baada ya na Marekani
kuingilia kati.
Mnamo mwaka 1948 Castro alimuoa Mirta
Diaz-Balart, mwanae mwanasiasa tajiri nchini Cuba. Mbali na kumtia
msukumo wa kujiunga na wasomi wa nchi, aligeuka kuwa na itikadi za he
Kimaxist Castro alikamatwa na kufungwa baada yauvamizi wake dhidi ya Moncada Garrison kushindwa mnamo mwaka 1953
Aliamini matatizo ya Cuba ya kiuchumi yalikuwa ni
matokeo ya ubepari usioweza kudhibitiwa ambao unaweza kutatuliwa tu kwa
mapinduzi.
Baada ya kuhitimu masomo Castro alizindua shughuli za
kisheria lakini zilishindwa kufanikiwa na aliendelea kuingia katika
mzozo wa madeni.
Alisalia kuwa mwanaharakati wa kisiasa, akishiriki katika misururu ya maandamano ya mara kwa mara ya ghasia.
Mnamo mwaka 1952 Fulgencio Batista alifanya mapinduzi ya kijeshi yaliyomg'oa madarakani rais wa Cuba , Carlos PrÃo.
Sera ya Batista ya uhusiano wa karibu na Marekani na kukandamiza
mashirika ya kijamaa vilikuwa pingamizi kwa kwa imani za kimsingi za
siasa za Castro.
Baada ya kushindwa kisheria, Castro alibuni
shirika lililoitwa The Movement, lililoendesha shughuli zake kisiri kwa
lengo la kuung'oa madarakani utawala wa Batista.
Cuba palikuwa
mahala pa watu matajiri kujivinjari, na nchi iliongozwa na kiasi kikubwa
na magenge ya wahalifu . Ukahaba ,wacheza kamali na walanguzi wa
mihadarati vilikithiri. Castro (Kushoto) akiwa na Che Guevara wakati wa vita vya msituni
Mwezi Julai 1953 Castro alipanga shambulio dhidi ya
kituo cha kijeshi cha Moncada akaribu na Santiago ili kupora silahga
kwa ajili ya kuzitumia katika harakati za kivita.
Shambulio
lilishindwa na wanamageuzi waliuawa ama kukamatwa . Castro alikuwa mmoja
wa wafungwa kadhaa waliofikishwa mahakamani mnamo mwezi Septemba
1953.
Castro alitumia muonekano wake mahakamani kutangaza maasi
yaliyotekelezwa na jeshi jambo ambalo baadae lilimpatia umaarufu,
hususan miongoni mwa waandishi wa habari wa kigeni ambao waliruhusiwa
kuhudhuria kesi hiyo.
Guerrilla warfare
Alihukumia kifungo
cha miaka 15 jela . Baadae aliachiliwa hru kufuatia tangazo la huruma la
jumla mnamo mwezi Mei 1955 baada ya kutumikia kifungo hicho kwa miezi
19 pekeekatika mazingira bora kiasi.
Katika kipindi hiki kifupi gerezani alimtaliki mkewe na kujiimarisha zaidi katika sera za kimaxist.
Kutokana
na Batista kuendela kuwakamata wapinzani wake , Castro alitorokea
Mexico kuepuka kutuwa nguvuni . Huko alikutana na mwana mageuzi kijana
aliyeitwa Ernesto "Che" Guevara.
Mnamo mwezi Novemba 1956,
Castro alirejea Cuba akiambatana na wanajeshi 81 akwenye ndege
iliyokuwa na uwezo wa kuwabeba watu 12 pekee. Vikosi vya Castro viliingia Havana mwaka 1959
Makao makuu ya chama yalitafuta hifadhi katika
milima ya Sierra Maestra . Kutoka kwenye ngome hii Castro alizingua
vita vya msituni dhidi ya utawala wa Havana.
Tarehe 2 Januari, 1959, jeshi la waasi likaingia katika mji mkuu wa Cubanna Batista akatoroka.
Mamia ya wafuasi wa zamani wa Batista walinyongwa baada ya kesi ambazo wageni wengi waliziona kuwa hazikuwa za haki.
Castro ralijibu kwa kusisitiza kwamba " Haki ya mageuzi haina misingi
ya kisheria ya kubadili tabia ama mawazo , bali inazingatia uwajibikaji
wa maadili ".
Serikali mpya ya Cuba iliahidi kurejesha ardhi kwa watu na kulinda haki za maskini.
Lakini mara moja serikali ilianza kulazimisha mfumo wa chama kimoja cha
kisiasa . Mamia ya watu walitupwa jela na kwenye kambi za kutumikisha
kazi za sulba kama wafungwa wa kisiasa.
Maelfu ya waCuba hususan wenye kipato cha kadri wakalazimika kuikimbia nchi yao. Castro alidai alilazimishwa kuingia katika muungano wa USSR wa Nikita Khrushchev
Castro alisisitiza kwamba fikra zake zilikuwa ni bora zinajali kwanza maslahi ya watu wa Cuba.
"hakuna ujamaa au umaxist , bali uwakilishi wa demokrasia na haki ya kijamiikatika mpango bora wa uchumi ," alisema wakati huo.
Mnamo 1960, Fidel Castro naliwapatia uraia wamarekani woote waliokuwa wanamiliki biashara katika kisiwa hicho.
Kujibu hatua hiyo, utawala wa Washington ulimuwekea vikwazo vya kibiashara vilivyo tarajiwa kudumu kwa karne ya 21st century.
Castro
alidai kuwa alilazimishwa kuingia katika mikono ya muungao wa Usovieti
na kiongozi wake , Nikita Khrushchev, ingawa baadhi ya wachanganuzi
walisema aliingia katika muungano huo USSR kwa utashi wake mwenyewe.
Iwe sababu yoyote ile, taifa la Cuba liligeuka kuwa uwanja wa mapamabano ya vita baridi vya dunia.
Mwezi
Aprili 1961, Marekani ilijaribu kuipindua serikali ya Castro kwa
kuwapatia mafunzo wanajeshi binafsi wa Cuba waliokuwa ukimbizini ili
kuvamia kisiwa hicho. Castro akiruka kutoka kwenye kifaru wakati wa uvamizi wa jumps eneo la mwambao la Pigs
Katika mwambao wa Pigs,vikosi vya Cuba vilikabili
majeshi ya uvamizi , na kuwauwa wengi huku 1,000 wakikamatwa. Fidel
Castro alikuwa ameonja malaka kwa njia ya damu kwa hivyo asingeweza
kuwasamehe.
Mwaka mmoja baadae, ndege za uchunguzi za Marekani
ziligundua makombora ya Usovieti wakati zilipokuwa njiani kuelekea
maeneo ya Cuba.
Dunia ilishtushwa na uwezekano wa kutokea vita vya nuklia .
"msururu
wa maeneo yenye makombora ya masafa marefu ya kivita sasa yanaandaliwa
katika kisiwa kilichofungwa. Lengo la ngome hizi za makombora haliwezi
kuwa lingine zaidi ya kutoa uwezo wa kufanya mashambulio ya nuklia dhidi
ya mataifa ya magharibi ," alionya rais John F Kennedy.
Mataifa
yenye nguvu duniani yalibaki kushuhudia kinachoendelea lakini ni rais
Khrushchev pekee ambaye aliweza kuchukua hatua kwanza na kuondoa
makombora yake nje ya Cuba baada Marekani kukubali kuondoa kisiri silaha
zake kutoka Uturuki.
Fidel Castro, hata hivyo , alikuwa tayari ni
adui wa Marekani namba moja. Maafisa wa ujasusi wa Marekani CIA
walijaribu kumuua , katika kisa kilichojulikana kama -Operation Mongoose
ambapo mbinu mojawapo ilikuwa apewe sigara iliyokuwa imesheheni
vilipuzi. Castro alibaki kuwa maarufu miongoni mwa watu wengi wa Cuba
Mbinu nyingine zilikuwa za kushangaza , ikiwemo
mojawapo ya kumfanya ndevu zake zianguke ili kumfanya awe na sura ya
kuto heshimika.
Muungano wa Usovieti ulimwaga pesa ndani ya Cuba.
Ulinunua mavuno ya sukari inayozalishwa kisiwani humo na meli zake
kurejea na zimesheheni na bidhaa nyingine, kama vile chakula kilichokua
kinahitajika ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani vya biashara.
Licha
ya utegemezi wa msaada kutoka mataifa ya Usovieti , Castro aliiongoza
Cuba kuwa taifa jipya lisilokuwa na mafungamano yoyote.
Hata
hivyo, aliegamia hasa Afrika, ambako alituma majeshi kuunga mkono
wapiganaji wa msituni waliokuwa na sera za kimaxist katika nchi za
Angola na Msumbiji.
Kati kati ya miaka ya 1980 , hata hivyo,
siasa za dunia za maeneo zilibadili mkondo wake . Ilikuwa ni enzi ya
Mikhail Gorbachev, sera za glasnost na perestroika, na zilidhihirika
wazi kuwa kinyume na mageuzi ya Castro.
Utawala wa Moscow ukakata uhusiano wa kiuchumi maramoja na Cuba kwa kukataa kata kata kununua sukari ya Cuba. Papa John Paul II akisalimiana na Fidel Castro
Akiwa bado chini ya vikwazo vya Marekani na kukatwa
kwa huduma muhimu za mataifa ya Soviet , uhaba wa kudumu wa bidhaa na
ukosefu wa akiba ya bidhaa vilidhihirika ndani ya Cuba
Jazba ilipanda huku misururu ya kupata ikiendelea kurefuka.
Taifa ambalo Fidel Castro aliita lililoendelea zaidi duniani, hali ya maisha ilikuwa mbaya.
Katika
kati ya miaka ya -1990s, waCuba wengi walikuwa wamechoshwa na hali
nchini mwao. Maelfu walianza kutoroka kupitia njia ya maji hadi
Florida wakiwa na ndoto ya kuishi maisha bora zaidi. Wengi walikufa
maji, lakini ilikuwa kura tosha ya kutokuwa na imani na Castro.
Hata
hivyo Cuba ilirekodi baadhi ya mafanikio ya kufurahisha ndani ya nchi.
Huduma bora za matibabu zilitolewa bure kwa wote , na viwango vya vifo
vya watoto wachanga wa vililinganishwa na vile vya mataifa tajiri
duniani.
Katika miaka iliyofuata , Castro alionekana mtulivu .
Mwaka 1998 alitembelewa na Papa John Paul II, jambo ambalo halingeweza
hata kufikiriwa miaka mitano ya awali.
Wakati huo Papa aliilaumu
Cuba kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu , na kumuaibisha Castro
mbele ya vyombo vya habari vya dunia.
Fidel Castro alikuwa
amebuni utambulisho wake kama mjamaa wa Caribbean ambao kwa miaka kumi
iliyopita , alilazimika kuukumbatia , pole pole alianzisha mabadiliko
machache ya biashara huria ili kulinda mageuzi yake.
Tarehe 31
Julai 2006,siku chache tu kabla ya maadhimisho ya mwaka wake wa 80 wa
kuzaliwa, Castro alikabidhi mamlaka ya muda kwa Raul baada ya kufanyiwa
upasuaji wa dharura wa utumbo.
Afya yake iliendelea kudhoofika.
Mapema mwaka 2008, Castro alitangaza kwamba hatakubali nyadfa za urais
na amiri jeshi mkuu katika mkutano kuu ujao wa kitaifa.
Katika barua iliyochapishwa katika gazeti rasmi la kijamaa, alikaririwa
akisema kuwa : " Ni kudanganya nafsi yangu kuchukua majukumu
yanayohitaji kutembea na kujitolea , wakati siko katika hali ya kimwili
inayoniruhusu kufanya hivyo ." lijiondoa kwa kiasi kikubwa katika maisha ya umma ,
huku akiandika taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya
kitaifachini ya kichwa cha habari...Tathmini ya maisha ya amir Fidel.
Alijiondoa kwa kiasi kikubwa katika maisha ya umma ,
huku akiandika taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya
kitaifachini ya kichwa cha habari...Tathmini ya maisha ya amir Fidel.
Alijitokeza
tena mwezi Julai 2010, alipoonekana mbele ya umma tangu augue,
akiwasalimia wafanyakazi na kuhojiwa na televisheni ambapo alijadili
kuhusu hali ya wasi wasi baina ya Marekani na Iran pamoja na Korea
kaskazini.
Mwezi uliofuatia Castro alitoa hotuba yake ya kwanza
katika bunge la taifa baada ya miaka minne, akiitaka Marekani kuacha
kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran au Korea Kaskazini akionya
kutokea kwa maafa ya nuklia ikiwa uhasama utazidi.
Alipoulizwa a
ikiwa Castro anaweza kuingia tena katika serikali , waziri wa utamaduni
Abel Prieto aliiambia BBC: "nadhani wakati wote amekuwa katika maisha
ya siasa za Cuba lakini hayuko serikalini. Wakati wote amekuwa makini
kwa hilo. Vita vyake vikuu ni kuhusu masuala ya kimataifa."
Tangazo la rais Obama la Disemba 2014 la mwanzo wa kumalizika kwa
vikwazo vya Marekani vya biashara na vinginevyo lilionekana kama
matumaini katika kile kilichokuwa uadui wa nusu karne uhusiano baina
ya nchi hizo mbili.
Castro aliafiki hatua hiyo aliyoielezea kuwa "
hatua nzuri ya kutafuta mani ya kikanda ", lakini hakuiamini serikali
ya Marekani.
Wakati waCuba wengi bila shaka hawakumpenda Castro,
wengine walimpenda kwa dhati . Walimuona kama David ambaye aliweza
kukabiliana na Goliath wa Marekani.
Kwao Castro alikuwa Cuba na Cuba ilikuwa Castro.
Historia ya Fidel Castro
Reviewed by Nurdidy
on
12:02 AM
Rating: 5
No comments