Breaking News

Magufuli avunja mwiko JWTZ

Kwa miaka yote, marais waliopita walikuwa wakisafiri kwenda Monduli mkoani Arusha kuwatunuku nishani maofisa wanaomaliza mafunzo yao, lakini jana Rais Magufuli alitunuku kamisheni kwa kundi la 59 la maofisa wapya 194, wakiwamo wanawake 26 na wanaume 168, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Siri ya uvunjaji mwiko?
“Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao?” Alibainisha Rais Magufuli kupitia taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
“Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu."

No comments