Breaking News

Takukuru nayo yafumuliwa


Mabadiliko hayo yanafanyika ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu Rais John Magufuli alipomwondoa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani na kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Nafasi ya DCI na ile ya Takukuru shughuli zake kwa kiasi kikubwa zinarandana, isipokuwa tu ile ya Takukuru imejikita kwenye rushwa wakati nafasi hiyo nyingine inahusu makosa ya kihalifu yote.
Hivyo ni wazi kuwa mabadiliko hayo, kwa pamoja, yanalenga kusuka upya vyombo hivyo ili kukabiliana na wimbi la uhalifu linalokua kwa kasi.
Taarifa kutoka ndani ya Takukuru ambazo gazeti hili ilizipata juzi, zilisema mabadiliko hayo yamefanywa na Mkurugenzi Mkuu, Kamishna Valentino Mlowola, ikiwa sehemu ya kuboresha utendaji kazi.

No comments