Breaking News

Man utd mbioni kumsajili Mikel Obi

Kocha wa Manchester united ambaye kwasasayupo kwenye presha kubwa kufuatia matokeo mabovu ya timu yake hiyo anayoifundisha kwasasa yuko mbioni kuendelea kuimarisha kikosi cha klabu hiyo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kiushindani.
Kwasasa kocha huyo ameelekeza mipango yake kwa klabu ya Chelsea ili kuweza kumsajili kiungo wa timu hiyo ambaye kwasasa hapati nafasi sana klabuni hapo Mikel Obi raia kutoka barani Afrika nchini Nigeria'.
 Mourinho anamfahamu vizuri mchezaji huyo kwani aliwahi kufanya naye kazi akiwa na klabu ya Chelsea na anaamini kumpata mchezaji huyo kutamsaidia yeye kuweza kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo kwasasa imekuwa ikimnyima usingizi.
 Hilo huenda likafanikiwa kirahisi kwani mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Chelsea unaisha mwishoni mwa msimu huu ingawa kuna klabu nyingine kama inter Milan zimeonyesha nia ya kumhitaji.

No comments