Manchester utd yatibuliwa ushindi dakika za lala salaama.
Klabu ya soka ya Manchester united imejikuta ikizidondosha pointi 2 katika uwanja wake wa nyumbani dakika za lala salaama baada ya klabu ya Arsenal kusawazisha bao dakika ya 89 ya mchezo.
Katika mchezo huo klabu ya Manchester united ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kiungo wake raia wa Hispania Juan Mata dakika ya 68 kipindi cha pili.Katika mchezo huo ambao k kwa kiasi kikubwa ulimilikiwa na Arsenal ambao walinekana kucheza mpira mwingi huku wakishindwa kutengeneza nafasi ya kufunga.
Manchester united pamoja na kwamba hawakuweza kumiliki mpira lakini walionekana kuwa hatari zaidi wanapofanya mashambulizi langoni mwa adui.
Katika mchezo huo kocha wa Manputd alionekana kuhuzunishwa na kitendo cha mwamuzi kutowapa penati tilu yake akiamini kuwa haki haikutendeka.
Kwa matokeo hayo hali inaonekana kuwa bado ni tete kwa klabu ya Man utd wanaotaka kurudisha heshima ya klabu hiyo ambayo imepotea kwasasa.
| Mourinho akipeana mkono na Wenger leo baada ya mechi |

No comments