Raisi Magufuli amefanya uteuzi mwingine TCRA
Rais John Pombe Magufuli amemteua Dk Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Slyvester Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 17 Novemba, 2016.
Taarifa hiyo imeletwa na Ofisi ya Mawasiliano ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, jana ilieleza kuwa Waziri uteuzi huo unaanza mara moja .
Kadhalika, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa (Mb) amewateua Valerie Ndeneingo Sia Msoka, mwanahabari, Dk Jabir Kuwe Bakari, Mtendaji Mkuu, Wakala wa Serikali Mtandao, Dar es Salaam kuwa wa jumbe wa bodi ya TCRA.
Wajumbe wengine ni Wakili Butamo Kasuka Philip, Meneja wa kampuni ya uwakili wa Top Attorney na Suleiman Mndewa, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar.
Uteuzi wa wajumbe hao ni kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Na. 12 ya Mwaka 2003. Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba,

No comments