Breaking News

Yanga yamtambulisha rasmi Lwandamina mbele ya Pluijm.


Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, George Lwandamina ametua kikosini hapo na kukabidhiwa jukumu la kuinoa klabu hiyo akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans Van der Pluijm aliyepewa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati wa utambulisho wa wakuu wapya wa Idara ya Ufundi, Lwandamina alisema kwamba hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi la Ufundi.
Na kuhusu kuongeza wachezaji, Lwandamina amesema kwamba ameiona Yanga katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikishinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na amegundua ni timu nzuri ambayo haihitaji mchezaji mpya.

No comments