Tottenham wameondolewa kwenye michuano ya Ulaya kwa kipigo cha 2-1
Klabu ya soka ya Tottenhqm ya nchini uingereza imeondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa klabu ya nchini Ufaransa,Monaco.
Katika mchezo huo klabu ya monaco iliweza kutawala mchezo hasa kipindi cha kwanza na kuwafanya Tottenham kuonekana timu chovu na yenye ushindani duni.Ilikua ni dakika ya 48 mchezaji Dijbril Sidibe aliweza kuiandikia klabu ya monaco goli la kwanza na baadaye mchezaji Harry Kane akaisawazishia Tottenham goli hilo kwa kufunga kwa njia ya penati katika dakika ya 52.Dakika moja baadae Monaco wakaandika bao lao la pili na la ushindi kupitia kwa Thomas Lemar.
MSIMAMO ULIVYO KUNDI E
| # | Team | Pl | W | D | L | F | A | GD | Pts |
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1. | Monaco | 5 | 3 | 2 | 0 | 9 | 4 | 5 | 11 |
| 2. | Bayer Leverkusen | 5 | 1 | 4 | 0 | 5 | 4 | 1 | 7 |
| 3. | Tottenham Hotspur | 5 | 1 | 1 | 3 | 3 | 5 | -2 | 4 |
| 4 | .CSKA Moscow | 5 | 0 | 3 | 2 | 4 | 8 | -4 | 3 |
No comments