Wapinzani DRC kuanzisha kampeni kumtoa raisi Kabila madarakani
Kundi la wanaharakati nchini DR
Congo limeanzisha kampeni mpya ya kumshinikiza rais Joseph Kabila
kung'atuka mamlakani kulingana na ripoti za BBC Afrique.
Muhula wa
pili wa kabila na wa mwisho kwa ujumla unakamilika tarehe 19 Disemba na
wapiga kura wanatarajiwa kushiriki katika shughuli hiyo mnamo tarehe 27
Novemba ili kumchagua mrithi wake,lakini makubaliano ya kisiasa
yalioafikiwa mwezi uliopita na kundi moja la upinzani yaliahirisha
uchaguzi huo hadi mwezi Aprili 2018.Lakini ukipinga makubaliano hayo muungano wa vuguvugu la kidemokrasia ulizindua kampeni ya ''Bye-Bye Kabila'' ili kumshinikiza kung'atuka muhula wake unapokamilika mwezi Disemba.
Mavuguvugu yalio nyuma ya kampeni hiyo -Filimbi,Lucha na Jeunesse du Rassemblement yamesema kuwa yataandaa maandamano dhidi ya serikali.
Hatua hiyo huenda ikasababisha makabiliano makali na vikosi vya usalama.
Mnamo mwezi Septemba,msako dhidi ya wale wanaoipnga serikali ulisababisha vifo vya watu 50.
Marie-Joel Essengo,kiongozi wa vuguvugu la Lucha aliambia BBC Afrique:Tutafanya maandamano ili kuwahamasisha miongoni mwa vijana ,katika uma wote hadi tutakapopata mabadiliko tunayohitaji.
Hatuwezi kusubiri na kufikiria kwamba bw. Kabila atepewa dakika moja ya ziada kuwa rais baada ya tarehe 19 Disemba.
No comments