WHO yatoa mwongozo mpya wa kujipima UKIMWI
Kuelekea siku ya UKIMWI duniani Desemba 01, Shirika la Afya Duniani
(WHO) limetangaza mwongozo mpya wa kujipima Virusi Vya Ukimwi, VVU kwa
lengo la kupanua upatikanaji wa huduma hiyo na uchunguzi wa virusi
hivyo.
Mwongozo huo unahusisha mtu kuchukua vitendanishi na kujipima kwa kutumia majimaji ya mwilini au damu kutoka kidoleni na kubaini iwapo ana virusi au la, na majibu anapata ndani ya dakika 20 au chini ya hapo.
WHO inasema iwapo majibu yanakuwa chanya, mtu huyo analazimika kwenda kituo cha afya na kusaka uhakika wa matokeo hayo ambapo ikiwa yatathibishwa, atapatiwa ushauri nasaha na huduma nyingine za matibabu ikiwemo dawa.
WHO inasema mwongozo mpya ni muhimu kwa kutafungua milango zaidi kufikia watu wengi na ni njia mojawapo ya kuwapatia watu uwezo juu ya afya zao na kusogeza huduma karibu na wananchi.

No comments